MH.RAIS KILIO HIKI CHA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU UMEKISIKSIA?
Naanza kwa kumnukuu aliyakuwa Wazili wa Uingeleza miaka 130 iliyopita Bw.Benjamini Disraeli alisema hivi “Hatima ya nchi hii (Uingeleza) Inategemea elimu ya watu wake” mwisho wa kunukuu. Hivyo hivyo na mimi nasema hatima ya Taifa changa kama la Tanzania inategemea elimu ya watu wake.Hivyo basi hatunabudi kujitahidi kadri ya uwezo wetu kuhakikisha kuwa kila mwenye bidii na ari ya kujiendeleza kielimu anapata fursa hiyo kwa kuwezeshwa aidha kifedha au kimawazo sana kifedha.
Mnamo April 2004 Bunge letu tukufu la Muungano lilipitisha sheria ya kuundwa kwa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu,kwa kisingizio cha kupanua udhamini wa selikali katika Elimu ya juu. Mnamo tarehe 20 aprili 2004 Wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam sehemu ya Mlimani na wenzao wa wenzao wa chuo kikuu kishiliki cha Ardhi waliamua kugoma kuingia madarasani na kufanya maandamano ya Amani ya kupinga kile walichokiona ni uonevu na ubaguzi wa Elimu kwa watoto wa wakulima wa Tanzania. Kwa mtazamo wao lengo la mandamano yao halikuwa kupinga muswada wa shelia ya kuanzishwa kwa bodi ya mikopo bali ni kukataa baadhi ya vifungu ambavyo mpaka sasa vinawaumiza. katika maelezo waliyoyatoa kwenye vyombo vya habari walionyesha wasiwasi wao mkubwa kwa Selikali kujitoa katika kugharamia Elimu ya juu,Jambo ambalo ndo chanzo cha migogoro ya mikopo mpaka sasa. Polisi bila yao kujua kwamba hawa wanafunzi wanaandamana kwa masilahi ya wototo wao wenyewe wakayazuhia maandamano hayo na kukamata baadhi ya wanafunzi. Hatimaye Chuo kikuu sehemu ya mlimani kilifungwa bila hata kufuatwa kanuni na taratibu za chou ambazo zinaelezea kwamba chuo kitafungwa endapo Mgomo utaendele bila kikomo au mfululizo kwa siku Tatu. Maamuzi ya kukifunga chuo yalipingwa vikali na wahadhili wa chuo hicho na kuamua kuwaunga mkono wanafunzi na hatimaye chuo kulifunguliwa na wanafunzi wote kurudi chuoni.
Kwa kuona hayo Selikali tarehe 22 Aprili 2004 kwa kupitia kwa wazili wa sayansi na Elimu ya juu wa wakati hule,iliamua kupeleka shutuma zake bungeni ikiwashutumu wanachuo hao na kufikia hatua ya kuwataja majina baadhi ya wanachuo.Katika utetezi wake Bungeni wazili alisema yafuatayo nanukuu “Mheshimiwa Spika tarehe 20 Aprili 2004 baadhi ya wanafunzi wakiongozwa na Bahati Tweve walianzisha maandamano kuelekea wizara ya Sayansi,Teknolojia na Eilimu ya juu.” Waziri aliendelea kusema “Mheshimiwa Spika kumeanza kujitokeza habari za kupotosha kwamba muswada unanufaisha matajiri au watoto wa vigogo.Tofauti na dhana hii potofu,lengo la muswaada huu ni kuunda chombo cha utoaji na urejeshwaji wa mikopo usiokuwa na riba ili kuwasaidia wanafunzi toka familia zenyekipato cha chini kama inavyobainishwa katika ibara 17(1) (d).Pili Muswaada huu unakusudia kuongeza idadi ya wanafunzi katika taasisi za Elimu ya juu”. Wazili aliendelea “Kumejitokeza wasiwasi miongoni mwa wanafunzi kwamba selikali imejitoa kugharimia elimu ya juu” aliendelea kufafanua “Gharama halisi za elimu ya juu kwa mwnafunzi ni wastani wa sh.1.6 milioni katika vyuo vikuu vya umma.Ada tu (tuition fee) ni wastani wa kati y ash.600,00/= na 1,000,000/=.Mwanafunzi atakopeshwa sh 600,000/= tu kwa ajili ya ada.Tofauti baina ya Gharama halisi na kiasi cha mkopo wa ada utakuwa ni Mchango wa selikali.”
Kwa maelezo hayo ya wazili Bunge lililidhika. Na ninadhani hata wewe Mh.Rais utakubaliana na mimi kwamba kwa maelezo hayo yaliyotolewa na Wazili huyo ulikuwa ni kutupaka Mafuta midomoni ili tuonekane tumekula vitumbua kitu ambacho si kweli. Katika maelezo hayo mazuri ya Wazili sisi sote tuliamini kuwa sasa kila mwanafunzi anayemaliza kidato cha sita ataenda chuoni,kiwe cha Umma au binafsi ili mradi kapata chuo.Tamko la Wazili Mwenye dhamana ya wizala ya Sayansi.Teknolojia na Elimu ya juu katika Selikali Yenye Kasi Mpya, Nguvu Mpya na Ari Mpya si tu lilitushangaza wengi bali lilituumiza vichwa wa Tanzania. Kabla hata hatujamaliza Matanga ya Tamko hilo la wazili Mh.Rais naye akapigilia msumari wa mwisho kwenye Jeneza la Elimu ya juu Tayari kupelekwa kwenye mazishi wakati aliyoko kwenye Jeneza hilo hajafa mbali na kelele nyingi alizozipiga yeye mwenyewe na jamaa zake.
Mh.Rais alipigilia msumali huo wa mwisho akiwa Mwanza alipokuwa akiongea na Wazee wa mwanza pale aliposema kuwa selikali itawakopesha wanafunzi wale waliopata Daraja la kwanza kwa upande wa Wavulana na Daraja la kwanza na la pili kwa Upande wa Wasichana.Kwa mtazamo wangu na jinsi tunavyokwenda upendeleo huu uliovishwa jina la Usawa wa kijinsia utatuponza uko mbeleni.Hapa naomba watu wanielewe mimi sipingi upendeleo huo ila napinga unavyotumiwa kama kigezo cha kumbagua mwingine kitu ambacho ni kinyume na Katiba ya nchi.maana yangu hapa ni kwamba suala hili litazamwe upya .Tunaposema Daraja la kwanza lazima tutofautishe ni katika masomo yapi kwa mfano masomo ya sayansi amboyo ndo msingi wa maendeleo ya Taifa lolote Duniani,kwa kutumia Mitaala au programu za ufundishaji tulizonazo ni vigumu sana kwa Mtu kupata Daraja la Kwanza,hapa sisemi mtu hawezi kupata daraja la kwanza hapana,wapo wanaopata lakini ni wachache tukilinganisha na huitaji wa wataalamu hao.Matokeo yake ni Kupungua kwa Wanafunzi wanaojiunga na Masomo ya Sayansi wa kidato cha Tano.Kila mwanafunzi kwa sasa anakimbila akasome masoma ya nadhalia(art) wakiwa na mtazamo wa kuwa wa kisoma hayo na kuongeza Somo moja la Dini(Divinity) watapata Daraja la Kwanza ambocho ndo kigezo cha kukopeshwa.
Lakini mbali na hilo wanakuwa hawajakwepa matatizo ya Mkopo.Hata na wale wanaopata mkopo Bado wanakopeshwa aslimia sitini tu (60%),sasa ndo nashangaa tena sana ebu jiulize hizi asilimia 40% zitatoka wapi?. Mh.Rais na selikali yako mnapaswa kulitambua kuwa hawa ni Watoto wa Wakulima wa Tanzania wanaoishi vijijini ambao mwaka huu walishindwa kupata hata Sh 50/= ya kununua chakula cha Mgao cha njaa.Leo hii watapata 40% ya gharama za Elimu ya juu.
Mh. Rais siku chache zilizopita nilipata Bahati ya kuongea na baadhi ya wanafunzi wa elimu ya juu,kwakweli si jambo la uongo.Mh.Rais vijana wanasema umewakatisha Tamaa,matumaini yao yote waliyokuwa wameyaweka kwako yanazidi kuyoyoma kili siku iendayo kwa Mungu.Mh,Rais labda ni kukumbushe wewe na selikali yako,Wakati shelia hii ya Bodi ya mikopo ya elimu ya juu inapitishwa selikali ilisema kwamba Shelia hii si Tu itawanufaisha wanafunzi walioko kwenye vyou vya umma bali hata na wale walioko kwenye vyou Binafsi.Lakini cha kushangaza hata wale walioko kwenye vyuo vya Umma wamekosa mkopo huo. Kwa mtazamo wa Watanzania waliowengi,mwanafunzi anapopata nafasi ya kujiunga (Admission) katika chuo Kikuu chochote cha umma huyo basi anastaili na anazosifa na vigezo vya kupata mkopo bila kujali ni daraja lipi.Vigezo vya ni dalaja lipi vinapaswa kupangwa na chuo husika kulingana na masomo au taaluma anayokwenda kuisomea mwanafunzi huyo bila kujali jinsia, rangi, Dini, wala kabila
Kilicho nifanya nikuulize Mh.Rais swali la je “kilio hiki cha wanafunzi wa elimu ya juu umekisiksia”? nimeamua kukuuliza swali hili kwa vile siamini kama kweli Mh.Rais umenyamaza kimya uku tukishuhudia vijana wetu waliokuwa wamepata nafasi za kusoma katika Chuo Kikuu cha Dar-es salaam na vyuo vingine nchini wananyimwa mkokpo kwa kisingizio cha Dalaja lipi bila kujali masomo ya mtu anayosoma,Na kuendelea kuwaona watoto na wadogo zetu wakirudishwa nyumbani uku selikali ikijigamba na misemo ya Maisha bora kwa kila Mtanzania. Sasa najiuliza Mh.Rais ni maisha bora kwa watanzania wapi? Hawa tuliowatoa vyuoni au wengine? Kama sio kuuziwa mbuzi kwenye gunia .
Sasa hivi tunanadi Muungano wa kisiasa wa Afrika Mashariki,uku wananchi na wadau mbalimbali wakilalamika kazi zote kwenye Mikoa ya Kanda ya Kasikazni kuchukuliwa na Wakenya.sasa Mh.Rais naomba niulize hivi tutaweza kweli kumudu ushindani ndani ya Muungano huo kama tunawanyima vijana wetu elimu ya juu.Kama kweli Watanzania tuko makini ,hili nalo litangazwe kama janga la Kitaifa au hiitishwe arambee ya kuchangia Elimu ya Juu kwa vijana wetu wenye moyo wa kusoma.Najua hatutaweza kuona madhala yake kwa sasa ila uko mbeleni tutajuta.
Tumezoea kuona matumizi mabaya ya mali ya umma,Tumeona Wabunge wakitaka kuongezewa mshahara na malupulupu,Tumeona yananunuliwa magari mapya ya kifahari(Shangingi) ya Mawazili,wakuu wa mikoa,Wabunge,Wakuu wa Wilaya pamoja na ya wakurugenzi wa idara mbalimbali za selikali.Ukipiga gharama za Gari moja pamoja na mafuta yake kwa miaka mitano Gari moja linauwezo wa kuwakopesha Wastani wa wanavyuo Kumi na Watano au Kujenga shule za kisasa za msigi Tatu mpaka Tano.
Baba wa Taifa Mwalimu Juliusi Kambarage Nyerere wakiti akilihutubia Bunge mwaka 1965 aliwahi kusema hivi nanukuu “Ufahari mwiko Tanzania,Taifa changa la Tanzania ambalo linaongozwa katika msingi wa ujamaa wa kiafrika katika kupigana na maadui wa Binadamu lazima lijiepushe na anasa,Ufahari na Utumiaji mbaya wa Fedha za Taifa”Mwalimu mara nyingi alisisitizia matumizi endelevu ya rasilimali za Taifa wala si Semina endelevu,na kwa kujua kuwa Taifa letu ni Masikini na changa aliamua Masomo ya Elimu ya juu yadhaminiwe na selikali au Yatolewe bure kwa Wanafunzi wenye nia ya Kusoma Mpaka hapo Taifa litakapo jitosheleza na watu wake kuweza kujimudu kimaisha.kwa Mtazamo huo ndo maana leo unawaona hao ambao walisoma kwa msaada wa Baba wa Taifa leo hii wanasahau hayo na kuanza kuwawekea vikwazo watoto wa Wakulima mbao hawakunufaika mwanzoni na Elimu hiyo ya Baba Wa Taifa kwa kisingizio cha Daraja la Kwanza na Usawa wa kijinsia.
Hapa kuna mambo mawili Jambo la kwanza ni Wale ambao wamenufaika na Elimu hii ya Bure sasa wangependa kuona Familia zao ndo zinanufaika na Mchakato mzima na Maliasili ya Taifa ,Kwa sababu wanajua watawapeleka Watoto wao kwenye Shule nzuri na zenye uwezo wa kutoa Daraja la kwanza uku wakijua fika kuwa shule za Watoto wa Wakulima ni zile za kutwa zilizojengwa kwa Nguvu za Wanznchi Zenye Walimu kati ya mmoja mpaka wanne, Shule ambozo hazina maktaba au kama zipo basi hazina vitabu vyote vya kiada na ziada,shule ambazo mwanafunzi anatembea Zaidi ya Kilometa Tano ndo Afike shuleni,Ebu jiulize hata kama angekuwa ana akili ya namna gani kweli huyo mtu ataweza kweli kupata Dalaja la Kwanza?. Pili hao ambao wamenufaika na huu mfumo wa Wachache wanawatengenezea mazingira watoto wao na wadogo zao ili baadae waje waongoze Taifa ambalo watu wake hawajui haki zao za msingi ili waenedeleze ule Msemo wa mwenye nacho ataongezewa.
Mh.Rais naomba ukae na Maprofesa uwaulize ni wangapi kati yao walipata Daraja la kwanza kidato cha Sita?Wewe tu anzia na Wazili mwenye dhamana ya wizala ya Sayansi na Elimu ya juu,kama watafika hata Robo au waulize ao wanaopanga viwango hivyo kwenye Bodi kama wao walipata Daraja la kwanza,alafu waulize ni kwanini wao wameamua kufanya hivyo? Waulize kama kweli wana mipango mizuri na Taifa masikini na changa kama hili?.Hivi hawa wametumwa na nani? Mbona Watanzania tunasifika kwa amani,umoja na Upendo.
,Mh.Rais usipoangalia hii la Bodi ya mikopo litatugawa na itafika hatua ya watu kukosa uvumilivu na kuamua kufanya mambo ambayo nisingependa yatokee Watanzania.Naomba niwakumbushe Kipande kidogo cha Hotuba ya Baba wa Taifa wakati wa Uhuru mwaka 1961 alisema hivi “Tutawasha mshumaa juu ya mlima Kilimanjalo uangaze ndani na nje ya Mipaka yetu,Ulete matumaini Pale penye kukatisha tama,Upendo penye chuki na heshima pale palipokuwa na dhalau” Sasa sijui kama mshumaa huu kweli bado unawaka make Naona Matumaini ya Watanzania yanayoyoma. Ni matumaini yangu kuwa Mh.Rais utaruhusu mshumaa huu uendele kuangaza kutokea mlima Kilimanjaro.
Namalizia kama nilivyoanza kwa kumnukuu aliyakuwa Wazili wa Uingeleza miaka 130 iliyopita Bw.Benjamini Disraeli alisema hivi “Hatima ya nchi hii (Uingeleza) Inategemea elimu ya watu wake” mwisho wa kunukuu. Hivyo hivyo na mimi nasema hatima ya Taifa changa kama la Tanzania hatima yake inategemea elimu ya watu wake.Hivyo basi hatunabudi kujitahidi kadri ya uwezo wetu kuhakikisha kuwa kila mwenye bidii na ari ya kujiendeleza kielimu anapata fursa hiyo kwa kuwezeshwa aidha kifedha au kimawazo sana sana kifedha.
0 Comments:
Post a Comment
<< Home