Tuesday, August 22, 2006

FILAMU YA MAPANKI ITAZAMWE UPYA


Tangu serikali ya awamu ya nne iingie madarakani mpaka sasa wananchi wamekuwa na matarajio makubwa kutoka kwa uongozi wa Rais Jakaya. Na sio tu kwa sababu ametoa ahadi bali ni kwa sababu ameanza kuzitekeleza kwa kasi na Ari na Nguvu mpya. Ukiangalia kwa kipindi kifupi amekuwa akijaribu kuvalia njuga kelo nyingi hasa zile za muda mrefu kama uwekezaji kwenye madini, selikali ya awamu ya nne imeamua kupitia upya mikataba ya uchimbahji wa madini ili nchi kama Taifa ifaidi maliasili zake.
Mimi ni kijana mdogo sana, lakini ukiniulizia kelo kubwa n ipi? nitakwambia ni ya wananchi wa Kanda ya Ziwa kula mabaki ya samaki yanayotoka kwenye viwanda vya samaki kwa lugha ya mtaani Mapanki.

Mimi msimamo wangu na ninasisitiza kuwa mapanki ni kitoweo cha kawaida na cha kila siku kanda ya ziwa sio Mwanza tu. Hata Bukoba wanakula Mapanki” bwana. Mimi mwenyewe nimeanza kula mapanki kuanzia mwisho mwa miaka ya tisini, Leo hii watu wanashangaa kitoweo cha Mapanki, ila nimejikuta nakula mapanki kutokana na uhaba wa sangara. Katika ziwa Victoria kuna mambo mengi sana ambayo hayajaanikwa adharini, mfano wavuvi wadogowadogo kutekwa na kunyanganywa samaki.
Sisi tulizoea kununua samaki kwa wachuuzi wadogowadogo ila kwasasa Hawapo, make wnakamatwa kwa kisinginzi eti Wanavua samaki wadogo. Sasa najiuliza hivi hawa wameanza kuvua samaki wadogo baada ya viwanda kuja? Saida Karori (mwanamuziki) aliimba wimbo uliokuwa unaonyesha au unaweka wazi unyanyasaji wanafanyiwa wavuvi wadogo wadogo, katika kibao cha Rugema Saida anaimba “Nsigire mbarwana, mbarwanira obukeije nobudagaa nzoenfulu eziango” maana yake, aliwaacha wanagombania Kambale na Dagaa ndo Samaki wakubwa. Anaendelea kuimba “Nganyila omusigazi, umusigazi, Rugema mbamwaka enfuluze ezeelufu Gashatu mbanaga umumaizi, Nibatela ebiboko” Saida Hapo anasema “Namuulumia Kijana, Kijana Rugema aliyenyanganywa samaki wenye samani ya shilingi 30,000/= samaki hao wakatupwa majini na yeye kuchapwa viboko. Saida anaendelea kuimba “Nauliza swali mvuvi na mchawi muovu ni nani?” Haya yote alikuwa anajaribu kuonyesha wazi unyanyasaji unaofanyika ndani ya kanda ya ziwa. Na haya ndo mambo yanayoonyeshwa kwenye filamu hii ya mapanki kama wanavyoiita.

Watanzania hapa lazima filamu hii itazamwe upya na ifanyiwe utafiti ili ukweli ujulikane kama mtunzi ana makosa au la. Au kama viongozi waliomdanganya Rais kwamba mapanki yanaliwa na watu maskini. Nasema Rais amedanganywa kwa sababu Rais Hakai Mwanza, viongozi wetu wa Mwanza ndo wamempotosha Rais kama walivyozoea kuwapotosha viongozi wengine wa kitaifa make Rais kama Rais hawezi kuelewa kila kitu. Viongozi wetu wa Mwanza wamejisahau wakadhani ni kipindi kile cha zidumu fikra za mwenyekiti wa chama zana ambazo wananchi walionyeshwa mbuzi kuwa ni Ngombe nao wakashangilia bila kuhojiwa ni kwa namna gani mbuzi ageuke kuwa Ngombe? Sasa wakati huo umekwisha henzi hizi ni enzi za zama za uwazi na ukweli, Hapa hatuwezi kubadili ukweli kwamba wananchi wa Mwanza wanakula mapanki kutokana na sangara kuadimika au kuwa bei ghari kwa sababu ya viwanda vya samaki ambayo havina faida kwa wananchi, ebu tujiulize kama viwanda vyenyewe haviwasaidie wananchi wa Mwanza ni bora vikafungwa watu wakaendelea kupata samaki kwa ajili ya kitoweo.

Nasikia huko Mwanza watu wameandamana kuonyesha wazi eti hawali mapanki hiki ni kichekesho cha mtu kuwa kasuku uku akijua. Na hii ni dhambi kubwa kuliko zote, kwa wale wakatoliki mnajua ya kuwa ukitenda kosa na uku unajua unafanya kosa basi kosa hilo linakuwa ni dhambi ya kifo. Hawa wananchi walitenda Dhambi ya kifo na wanatakiwa kutubu make wamekuwa wahongo. Hivi mtu unaandamana halafu unakopita unaona kabisa watu wanauza na kununua mapanki na unajua leo mkeo au mama yako nyumbani amepika mapanki huo ni uzalendo au ni ukasuku. Nelson Mandela aliwahi kusema kuwa kama msomi anayetegemewa na jamii unaponyamaza kimywa kwa kitu ambacho jamii inakiona kuwa ni kosa, lakini wewe unakishabikia unastahili kutupwa jela kwa kosa la jinai lililo kubwa kuliko kosa la uhaini” sasa hawa wasomi wenzentu wa Mwanza mbona mmekaa kimya au mnaendelea kuabudu msemo wa it is not my business au wa mind your own business.
Uku mkiendelea kuona uhovu unatendeka kwenye jamii. Na udanganyifu mkubwa ebu jiulize kama kweli mtayarishaji wa filamu hii aliingie nchini kwa utaratibu unaofaa, akawasilisha rasimu (script) ya alichokusudia kwenye vyombo husika na utaratibu wote ulifuatwa na ninafikili hata Wizara ya utamaduni iliachiwa nakala kama hawakuachiwa huo n uzembe,na kama waliachiwa kwa nini hawakulizungumzia suala hilo mwanzo mwa mwaka 2004 mpaka wasubili leo? Kama sio ukasuku ni nini? leo viongozi wetu wa mwanza wanajivisha ngozi ya kondoo wakati ndani sio. Tuwaelewaje. Wanafikia hatua hata ya kumdanganya Rais wetu, tunayemheshimu na kumtegemea sana kuliko Marais wowote waliopita Tanzania. Leo hii mnaanza kumdanganya kama mlivyozoea, mimi nafikili za mwizi zimekalibia, zama za kukwepa ukweli zimekwisha hii ni Ari mpya, Kasi mpya na Nguvu mpya.

Nawaomba Wabunge wa Kanda ya Ziwa mlichukulie uzito swala hili. Ila naomba mfanye utafiti kwanza kabla hamjalizungumzia make mimi naamini kwenye philosofia ya no research no right to speak”
Filamu kama Filamu naweza kuwa na mapunguvu; hilo mimi sikatai hivyo kwa sababu suala la kwamba Ndege zinazopeleka samaki zinakuja na siraa, hilo siwezi kulizungumzia kwani nina imani kubwa ya ulinzi tulionao tena wa kisasa kwenye viwanja vya ndege ukizingatia ni hivi karibuni tumetoka kununua Rada kubwa. Hila kama kweli ndege hizo upitia kwanza Congo na Sudani, hilo liko nje ya uwezo wetu na hilo ni kosa kubwa kulihusisha na Tanzania.
Suala la mabinti kujiuza hilo halina ubishi wanajiuza kweli kweli. Hata juzi tu mkuu wa mkoa wa Dar – es – salaam amewafukuza kwenye viota vyao. Ilo suala la mabinti kujiuza liko Duniani kote na katika nchi za ulaya wanachangia kwenye uchumi wa nchi husika, sehemu kama Asia limekuwa ni kivutio kwa watalii. Na uku Arusha wapo wanajiuza mtu akipenda aje nimpeleke wanakojiuza aone. Ila hilo suara haliusiani na suala la mapanki au Sangara au viwanda vya Samaki, ingawa kwa upande wa mtayarishaji hapo anaweza kuwa alitaka kuonyesha jinsi gani umaskini ulivyokidhili Mwanza na jinsi minofu ya samaki mbali na kuuzwa kwa Bei ghari ulaya haiwasadii watu wa Mwanza kuondokana na Uamaskini mkubwa walionao wananchi wa Mwanza.
Mara nyingi nasisitiza kwenye philrophy ya “no research no right to speek” tunapozungumzia jambo bila utafiti. Eti kupenda kujionyesha kwa mkubwa wetu huo ni ukasuka sio uzalendo na litaifikisha pabaya nchi yetu. Hapa mtu haitaji kuvaa miwani kuona uovu uliokidhili kwenye viongozi wa ngazi za chini mpaka wamefikia hatua ya kumpotosha Rais eti wanaokula mapanki ni watu maskini. Wakati hata wao wenyewe wameishawahi kula. Huo ni undumila kuwili au ukasuku. Hapa hapaitaji hubishi ukweli ni kwamba mh. Rais mapanki yanauzwa sokoni. Lakini hapa naomba nieleweke vizuri, mapanki yanayouzwa hayajaoza kama filamu inavyoonyesha lakini ukweli ni kwamba yanauzwa.

Hayati Mwalimu Nyerere aliwahi kusema katika mkutano mkuu wa TANU uliofanyika Mwanza tarehe 16th oktoba 1967 alisema hivi “Haina maana kwa kiongozi kuelewa takwimu kabra hajatambua kuwa Tanzania ni maskini na haina maana ya kujidanganya kuwa jambo Fulani, hasa umaskini haupo au wakati mwingine watu au viongozi uchanganya mambo kwa kutazama watu wachache wanaondesha magari yao binafsi na kuamini kuwa nchi ni tajiri” nimetoa mfano huu make ni viongozi wengi wenye mtazamo kama huo, kama kiongozi mmoja wa juu kwenye serikali ya hawamu ya tatu aliyesema eti hakuna mtanzania yeyote anayeweza kukosa kupata sh 500/= kwa siku. Na hii nairinganisha na hao wanaosema watu wa Mwanza hawali mapanki.Hapa lazima tuelewe ya kwamba matatizo yetu hayaweizi kuisha kwa kujifanya na kuamini kwamba hayapo au kuwa sababu tunawalaumu watu Fulani kuwa ndo chanzo cha matatizo, haisaidii lazima tuzitambue alama za nyakati hizi. Ndo maana nasema badala ya kumulaumu mtayarishaji wa Filamu ya Darwn’s Nightmare, tuchukue filamu hii kama changamoto la Taifa letu. Hapa tupende tusipende, tuwe wazalendo au tuwe na ukasuku wananchi wa Kanda ya Ziwa Victoria yaani Mwanza Bukoba na mara wataendelea kula mapanki. Na mimi nayasema haya kusudi viongozi wa serikali hasa wa Ngazi za chini ambao wanajivalisha Ngozi ya Kondoo kumbe ndani ni mbwa mwitu waliomdanganya Rais eti wanao kula mapanki Mwanza ni watu maskini wakati ukweli ni kwamba mapanki yanaliwa na watu wa kawaida hata maofisa wa serikali nao wanayala. kuwa suala hili hapa halina ubishi wowote hapa lazima Filamu hii itazamwe upya.

1 Comments:

At 2:11 AM, Blogger Simon Kitururu said...

Nakubaliana nawe kabisaaaaaaaaa!

 

Post a Comment

<< Home