MKO WAPI WANAMAPINZUZI NA WASOMI WETU?
“ Kama ningekuwa kijana ningeanzisha Mapinduzi “ aliongea Mzee wa mika 80. “Mapinduzi ya nini?niliuliza” ya kila kitu “ alijibu .
Watanzania walio wengi watakubaliana na mzee huyu kwa sababu katia ya watanzania watatu ( 3 ) unaokutana nao wawili (2) wanakiri kuwa kuna umuhimu wa kufanyika mabadiliko. Kama umma unapigania marekebisho yafanyike, mara nyingi wanapigania mabadiliko kwenye elimu, Afya, Kilimo, Maji, Sheria na Sera za kiuchumi. Katika nchi watu wanapingana dhidi ya ujinga , umasikini na maradhi lazima pawepo na kilio cha mabadiliko.
Katika nchi yeyote Duniani panakiwepo na Biashara isiyo na usawa , mamlaka ya sheria kutotoa haki , huduma mbaya za mahospitalini, Elimu yenye ubaguzi unyanyasaji wa kijinsia pamoja na ubaguzi wa kidini , kikabila na uchafuzi wa mazingira, yote haya yamewaacha watanzania wakilalamika .
Sasa tujiulize tufanye nini? Biblia inatambua “ Mtawatambua kwa matunda yao. Je Watu huchuma zabibu katika miiba au tini katika mibaruti? Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri na mti mwovu huzaa matunda mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matunza mabaya wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. Mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. Ndipo kwa matunda yao mtawatambua” Mt: 7:16-20 .
Kwa mtazamo huo huo, hata tukihubiri matatizo yaliyosababishwa na rushwa, watu kunyimwa haki zao za kimsingi , umaskini uliokithiri, uharibifu wa mazingira na mabo mengine. Mizizi yake ni mrefu zaidi kuliko tunavyofikiria. Kinachihitajika ni mabadiliko ya mfumo mzima. Tunahitaji Serikali itakayoleta mfumo mpya wa Kuongoza na kusimamia vizuri rasilimali za Taifa. Serikali itakayowapa wananchi Elimu bora, kazi , Nyumba, Chakula ( Kilimo chenye ruzuku ) Hospital zenye madwa na kuhifadhi mazingira.
Upande mwingie wa pili, kma kweli tunahitaji mabadiliko ya kweli ya kuwa na nchi isiyokuwa na rushwa , serikali isiyokuwa na matatizo niliyoeleza , ni lazima sisi wananchi tuwe tayari kubalika na si tu serikali ibadilike.Je Nauliza ni vijana wangapi wako tayari kubadilika? Na uliza Vijana. Tunapaswa kuwacha kuendelea kumlaumu Mungu, Kwa viongozi wabaya eti ni chaguo la Mungu, sisemi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Serikali yake ni viongozi wabaya la asha lakini kuna viongozi wengine waliochaguliwa kwa mkumbo wa chama ambao hawafai na wananchi wanawafahamu, Matokeo yake watampa shida Mheshimiwa Rais.
Embu fikiria kwa mfano, mti uanguke Mtu afe, watu watasema ni mapenzi ya Mungu , Je Mungu, ndo aliyesababisha Mti uanguke? Lazima tujiepushe na malalamiko ya kuwa Mungu anapenda tupate shida au anatujaribu, sio kweli matendo mengine ni matendo ya watu . Umeingia ugonjwa unaoitwa kwa kiingereza “Mind your own Business” Je lipi halikuhusu unataka kusema mali ya Umma haikuhusu? Kama kwili inakuhusu kwanini unaka kumya? Lakini hii imekuwa ni tabia ya watanzania make kila mmoja anaogopa kuitwa adui wa umma ebu fikilia kama tunaangalai mabibi zetu wanawatahiri watoto wa kike ili wawaongezee soko kwenye soko la ndoa, watoto wadogo wanaingizwa kwenye biashara ya mapenzi, tunakaa kimwa,kwa sababu ya ugonjwa wa “mind your own business’’,ni ugongwa kwa sababu unawafanya watu wanaumwa matokeo yake mtu akifa kutokana na matendo hayo yote, tunasema ni mapenzi ya mungu.Huku ni kufanana na Yuda Iskarioti na vipande thelathini 30 vya fedha.
Hakuna kitu chochote kisichowezekana lazima tuwe tayari na tujiandae kubadilika,lazima kwanza tubadilishe fikra zetu,na hii itachukuwa muda ,lazima tuondokane na zana haiwezekani kwenda inawezekana,haifanyiki kwenda inafanyika siko tayari kwenda niko tayari ili mradi yawe yanaleta mabadiliko katika nchi.Lakini tukumbuke mabadiliko yatakuja jinsi utakavyo jiandaa! Msemo wa wanafarisafa kwamba aliwazalo mjinga ndilo litakalo mtokea. Ukitaka kujua mabadiliko ya gafla yataiharibu jamii na mabadiliko ya taratibu sana yataidumaza jamii.Kabla ya Marekani na Wingereza kufikia hapa walipo ilichukuwa kipindi kirefu. Nina uhakika na sisi tutafika hapo siku moja. Lakini lazima tuanze kuwa na siasa za uvumilivu, siasa za kuwavumilia wenye mawazo tofauti na sisi, hasa mawazo ya kisiasa lazima tuvunje ukabila unaoanza kujitokeza kwa sasa ili tuweze kuendelea kiuchumi.Usiniulize kwa nini dini imeshindwa kutuunganisha? narudia madiliko yeyote ya yanachukuwa kipindi kirefu lakini tunaweza kuanza taratibu kuwachanganya watoto kutoka kwenye tabaka mbalimbali shule moja, kuwashawishi wafanya biashara kuwa wajasilimali ilikutoa ajira.
Yote haya yanahitaji mabadiliko kwenye siasa na sayansi, ilikubadilisha mfumo mzima wakijamii na kiuchumi ilituweze kutoka kwenye mfumo wa jana mpaka mfumo wa leo,kubadilisha fukra kutoka kwenye mtu mwenye kitambi na gari la kifahari kwenda kwenye mtu mwenye upeo wa mambo.Tusiwalaumu sana wazee wetu kwa hayo,kwasababu program wanayotumia ilifanikiwa katika miaka 1980 ya plan” A”.
Tukirudi nyuma tukatazama upande mwingine tunawaona vijana wengi tu na wasomi wako serikarini jiulize yako wapi mabadiliko?ziko wapi fikra na mawazo mapya ya kiuchumi na kijamii?Au hayawahusu!! “Non of their Business” ugonjwa usio na tiba. Uko wapi uwekezaji kwenye taharuma, teknolojia na uzalishaji kwa ajili ya Umma, mambo yatakayotusaidia kukuza Uchumi wa kesho? Ni nani wa kuanzisha Agenda hii? Nani anataka kuitwa adui wa Umma?
Labda tusiwalaumu wanaweza kuonekana ni vijana, kwa mavazi ya ujana kama mimi,lakini wakawa na mawazo yaliyofanya kazi miaka 1980, miaka ya plan “A” . Jiulize wako wapi viongozi wa kutuongoza kwenye Karne ya 21 au labda hawajazaliwa kwa nini hivi? Ukiwauliza vijana kwanini hawako msitari wa mbele kwenye uongozi na katika mabadiliko ya sera za Kiuchumi, Kisiasa na Kijamii! Wataguna ! Hatuwezeshwi” wazee hawatutaki vijana. Au hatujapata mtu wa kutuwezesha. Vijana kuwezeshwa ni sababu za kimsingi ya kusubiri? .Mahatma Gandhi alipojitokeza kwenye Siasa za India wakati Aridhi ikiwa chini ya Falme na milki za Kikoloni, je yeye alipata uwezeshwaje upi? Nani aliyemchangia pesa au nani alimpa msaada wa Kampeni? Au Nelson Mandela alipoanza kupambana na Tawala wa ubaguzi wa rangi mpaka akawakomboa wazalendo wa Africa ya Kusini nakuwaletea Uhuru ni nani alikuwepo kumwezesha au aliwezeshwa na nani au ni msaada gain walioupata wapigania Uhuru wetu walipoingia misutuni? Mbali na kutopata msaada waliishia Jela na Vizuizini na kutangazwa wasaliti hata kwa Jamii zao wenyewe.
Hebu niishie hapa, tunaishi kwenye nchi yenye Demokrasia, yenye Uhuru wa kuongea na Uhuru wa vyombo vya habari. Niliposema wakati wa Mapinduzi ni sasa sikuimanisha na wala sitaimanisha kwamba kila Kijana achukue jiwe aponde Vioo vya Magari barabarani au tuandamane Barabarani, siyo hivyo, na hivyo si maana yangu na wala hata siku moja sitaimanisha hivyo. Na kama kuna mtu mwenye fikra kama hizo ni mtu nwenye akili finyu na niwakubezwa ni mtu asiyetufaa katika Jamii ya sasa. Lazima vijana na tuwe na sera za mabadiliko ya Kiuchumi naya Kisayansi, lazima tujitokeze kupigania nafasi mbali mbali. Ingawa uchaguzi umeisha lakini tunacho cha kutusaidia au tunae mheshimiwa Rais upande wetu tusife moyo.La pili mwaka 2007 ni mwaka wa uchaguzi mkuu ndani ya chama cha mapinduzi{ccm}na kwa kadirio la chini kila penye watanzania watatu{3} wawili{2}watakuwa na umri chini ya miaka 40.Je tuna sera zipi za kuwapa watuchague ili tushike uongozi wa juu ndani ya chama?Je tuko tayari kuwa na mawazo ya mapinduzi ya kisiasa na kiuchumi?Amkeni wakati wa ukombozi ni huu!!
3 Comments:
Ningependa ujadili zaidi juu ya hoja ya "kubadili kabisa mfumo mzima wa maisha yetu." Watu wengi wakisikia neno mapinduzi wanadhani kuwa unaongelea uhaini, kubeba silaha au mawe kama ulivyosema. Nimefurahi kuwa umerushia vijana mpira, na kuuliza, unangoja nani akuwezeshe? Hii ndio sababu iliyonifanya kuita blogu yangu Jikomboe maana naamini kuwa sisi wenyewe tuna nguvu na uwezo mkubwa wa kujiwezesha. Ila kuna hii dhana ambayo tumejengewa kwa muda mrefu ya kusubiri watu wengine.
Jambo jingine ambalo nadhani ndugu Bwalya anaweza kuchangia ni pale uliposema kuwa tuache kumlaumu Mungu. Nakubaliana nawe. Ukikata miti ovyo, unakaribisha ukame. Mvua isipokuja unaanza kudai kuwa mungu ana gadhabu kutokana na dhambi zako. Ndio hii tabia ya kuhamisha kila kitu kwa watu wengine au nguvu zingine.
Lakini pale uliposema kuwa rais wa Tanzania yuko upande wetu ulikuwa una maana gani?
Kaka makala hii nakubaliana nayo kwa kiasi kikubwa. Suala la Mind yo own busness linaudhi na linakwamishasana masuala mengi. Kuna kauli nyingine siku hizi kuwa kila mmoja anataka cha juu!!!! Hapo namaanisha mazingira ya rushwa lakini hapo suala la uchaguzi wa CCM mwakani una maana gani?
Mzee hapo umenikuna kwelikweli.Tatizo ni kwamba ni watanzania wachache sana watakusikiliza. Unajua wengi watasema wewe ni mwanasiasa kwani hawajui bila siasa kama yako hakuna maendeleo.
Hongera sana, naomba pia ujaribu kuisoma globu langu.
Post a Comment
<< Home